Wasokotaji-hariri ni wadudu wadogo wa oda Embioptera (embios = -epesi, ptera = mabawa) ambao wana tezi kwenye miguu ya mbele zinazotumika kwa kusokota hariri. Hutumia hariri hii ili kuumba njia na vyumba juu ya miamba, juu ya gome la miti au ndani ya takataka za majani. Mwili wa wadudu hawa ni kinamo na una umbo wa mcheduara. Hii inarahisisha maisha yao ndani za njia za hariri. Madume ya spishi nyingi wana mabawa lakini madume ya spishi nyingine na majike wote hawanayo.
Wasokotaji-hariri huishi ndani ya njia za hariri takriban saa zote. Madume wanatoka njia hizi ili kutafuta majike, na majike wanatoka ili kutafuta chakula. Wakipata chakula majike wanaumba njia mpya za hariri juu ya chakula hiki. Hula takataka za majani, vigoga, gome na kuvumwani. Madume hawakuli.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili hazina jina kwa mnyama huyu au wanyama hawa.