dcsimg

Usubi (Ceratopogonidae) ( Swahili )

provided by wikipedia emerging languages

Usubi ni mbu wadogo wa familia Ceratopogonidae katika oda Diptera wanaofyonza damu. Spishi nyingi hueneza magonjwa kama vile mansoneliasisi, ugonjwa wa ulimi buluu na ugonjwa wa farasi wa Afrika. Kuna usubi wengine walio wana wa nusufamilia Phlebotominae katika familia Psychodidae. Usubi hao hufyonza damu pia na kueneza magonjwa. Halafu kuna usubi weusi wa familia Simuliidae ambao hueneza upofu wa mtoni.

Mbu hawa ni wadogo sana, mm 1-5. Rangi yao ni kijivu, hudhurungi, kahawia au kahawianyekundu. Macho ni meusi kwa kawaida. Mara nyingi toraksi (kidari) imepindika na kwa hivyo kichwa kinaelekea chini.

Chakula cha usubi ni mbochi, lakini majike wanahitaji damu ya mamalia, ndege au reptilia ili mayai yaendelee. Spishi fulani hufyonza “damu” ya wadudu wengine.

Usubi wengi, spishi za jenasi Culicoides hasa, ni vekta za magonjwa mbalimbali kama vile mansoneliasisi, ugonjwa wa ulimi buluu, ugonjwa wa farasi wa Afrika na virusi nyingi nyingine. Vekta ya ulimi buluu katika Afrika ya Mashariki ni Culicoides pallidipennis na labda C. cornutus, C. grahami, C. magnus na C. tororoensis pia.

Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki

  • Culicoides imicola
  • Culicoides nairobiensis
  • Culicoides pallidipennis
  • Culicoides schultzei

Picha

license
cc-by-sa-3.0
copyright
Waandishi wa Wikipedia na wahariri

Usubi (Ceratopogonidae): Brief Summary ( Swahili )